NEWS

29 Aprili 2020

Bei elekezi ya Sukari Yawaponza Wafanyabiashara Saba Wilayani Hai




Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Sabaya ameyafunga maduka saba wilayani kwake huku wamiliki  wakiwekwa chini ya ulinzi kwa kukiuka tangazo la Serikali kuhusu bei elekezi ya kuuza sukari.

Sabaya ametoa uamzi huo baada ya kufanya ziara ya kishtukiza leo Aprili 28, 2020 kwenye maduka hayo yaliyopo maeneo ya stendi kuu na kukuta sukari ikiuzwa kwa bei tofauti na iliyoelekezwa na Serikali hivi karibuni.

Aidha ametoa onyo kwa wafanyabishara wajumla katika wilaya hiyo kuuza sukari bei ambayo wafanyabisahara wadogo watauza  kwa bei elekezi.

Waliofungiwa maduka yao walikuwa wakiuza bidhaa hiyo kwa bei ya Sh3, 500 badala ya 2,700 iliyoelekezwa na Serikali mkoani humo