NEWS

29 Aprili 2020

Mrema amcharua mbunge Selasini kutoa sababu za kishamba kuhama Chadema


Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amemcharua Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kutoa sababu ya kishamba kuhama chama hicho.

Mbunge Selasini jana alitangaza kuhama Chadema na kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi huku akidai amefikia uamuzi huo baada ya kuondolewa kwenye grupu rasmi la kazi la WhatsApp Chadema bila kupewa sababu za kuondolewa.

Mrema aliandika ujumbe huu akimjibu Mbunge huyo kuwa ” Itakuwa mission ya kuscreen shot iliabort sio bure … Unawezaje kutoa sababu ya kishamba na kitoto kama hii?,”

Aliongezea kuwa “Lazima kulikuwa na kazi maalum inafanyika ndani ya group,” aliandika Mrema.

Mrema amesema waliokuondoa kwenye group la WhatsApp waliona mbali bila shaka ” Sitaki kuamini ulichosema Selasini,”.