Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA kimetoa maelekezo kwa Wabunge wake wote, kutohudhuria tena vikao vya Bunge vinavyoendelea,na wajiweke Karantini kwa muda wa siku 14 na wasiende majimboni kwao kipindi hiki mpaka pale watakapothibitika hawana maambukizi ya Virusi vya Corona
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe leo Ijumaa May 1, 2020 imetoa maelekezo manne kwa wabunge wa chama hicho ambayo ni; Kutohudhuria vikao vya bunge au kamati za bunge,Kutofika eneo la Bunge Dodoma na Dar es Salaam, Wabunge wajiweke karantini kwa muda wa siku 14, wabunge wa chama hicho wasiende mikoani au majimboni bali wabaki Dodoma hadi itakapothibitika hawana maambukizi
Aidha, CHADEMA pia wameshauri Bunge lisitishwe kwa siku 21 ili kuruhusu wabunge wote kwenda Karantini