NEWS

2 Mei 2020

Juma Lokole: “Jonijoo kaondoka Wasafi amemuogopa Lil Ommy, Hana ubunifu kipindi kimefutwa”



Mtangazaji wa Wasafi Fm @jumalokole2 amefunguka mengi sana kuhusu maisha yake ya Wasafi na maisha aliyokuwa kabla ya kujiunga na Wasafi.

Mbali na hilo @jumalokole2 amezungumzia sakata la kuondoka mfanyakazi mwezao @jonijooo ambaye amejiunga na Efm.
Juma ameongeza kuwa wao wanachojua ni kwamba Jonijoo aliambiwa aungane na @lilommy kwenye kipindi kipya akakaa kwa sababu kipindi chao cha jioni kilikosa mvuto huenda kwa sababu sio wabunifu.

Mbali na @jonijooo @jumalokole2 ametudokeza kuwa mmoja wa Watangazaji ambaye alikuwa akifanya kazi na Jonijoo nae ameshaondoka tayari Wasafi na kuna wengine watandoka.
Alipoulizwa kuhusu suala la maslahi alisema kuwa @jonijooo alishindwa kuitumia nafasi na Brand ya Wasafi kujiendeleza badala yake alibweteka na kusubiria mshahara tu.