NEWS

2 Mei 2020

Suma Lee Aahidi Kuwakutanisha Ali Kiba na Diamond Kwenye Qaswida Moja


Hitmaker wa Hakunaga, Sumalee, @hakunaga aahidi kuwaleta wasanii #Alikiba na #DiamondPlatnumz kwenye Qaswida moja.

Akizungumza leo Kupitia kipindi cha The Switch cha #WasafiFm, Suma Lee amesema miongoni mwa mambo anayohitaji kuyatimiza ni kuwaimbisha Qaswida wakali wawili wa Bongo Fleva #Alikiba na #DiamondPlatnumz

"Nitaimba Qaswida na Diamond pamoja na AliKiba, iwe Qaswida moja ama kila mtu na ya kwake... wataimba iwe kilazima, kihiari, nitaimba nao. Wataimba Qaswida". Alisema Maalim #Sumalee.

Itakumbukwa, kabla ya kuachana na #BongoFleva, #SumaLee aliwahi kutamba na kibao chake cha #Hakunaga lakini kwa sasa ana zawadi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan aliyoiachiwa mapema wiki hii inaitwa #YaRasulallah.