NEWS

1 Mei 2020

Lukamba: “Dodo ya Alikiba niliirudia mara tano, Nimependa Hamisa anavyomkumbatia Kiba”


Tulipata nafasi ya kupiga stori na Mpiga picha wa @diamondplatnumz @lukambaofficial na kufunguka mambo mengi sana.


Miongoni mwa mambo aliyofunguka ni pamoja na ukaribu wake na mama mtoto wa @diamondplatnumz @hamisamobetto.

Lukamba amezungumzia kuhusu wimbo wa @officialalikiba #DODO na kusema kuwa wimbo huo aliyangalia karibia mara 5 na kilichomfurahisha ni jinsi @hamisamobetto alivyokuwa anaenda kumshika @officialalikiba na hasa pale anapocheka.

Mbali na hilo @lukambaofficial amezungumzia kuhusu @tanashadonna na kusema kuwa akiwa kama shemeji yake amemmis sana maana ni mchangamfu sana.