NEWS

1 Mei 2020

Trump: Virusi vya Corona vilitengenezwa katika maabara ya China

Rais wa Marekani Donald Trump amedai kuwa ameona ushahidi kwamba virusi vya corona vilitoka katika maabara ya China.

Trump amesema hayo huku akitishia kuongeza ushuru kwa China kutokana na ilivyolishughulikia janga la corona ambalo limeukumba ulimwengu mzima.

 Hata hivyo, madai hayo ya Rais Trump yamekosa kutiwa uzito baada ya maafisa wa intelijensia pamoja na waziri wake wa mambo ya nje, Mike Pompeo, kusema kuwa hawajui kwa  ni wapi virusi hivyo vilianzia.

Ukosoaji wa hivi karibuni wa Trump dhidi ya China umejiri, huku takwimu zinaonesha kwamba Wamarekani milioni 30 wamepoteza ajira kufuatia masharti ya kutotoka nje.