NEWS

1 Mei 2020

Wasanii wa BONGO Watia Aibu..Rama Dee Adai Kupigwa Vizinga na Wasanii Kutoka Bongo

 

Msanii mkongwe na mkali wa RnB Rama Dee, amesema kutokana na tatizo la Corona nchini Australia, limemfanya kukaa ndani kwa  miezi miwili na kutokwenda kazini kwa muda wa miezi 6.


Rama Dee amesema licha ya kukaa ndani kwa muda wote huo, analipwa kama kawaida na kuna baadhi ya kazi za kiofisi anazifanya akiwa nyumbani, lakini anashangaa kuona kuna baadhi ya wasanii wanaachia kazi nzuri lakini bado wanamuomba pesa.

Akieleza hayo kupitia show ya Dadaz ya East Africa Tv, Rama Dee amesema muziki wa Bongo ni local sana na yeye binafsi ameacha kuimba miaka miwili iliyopita.

"Mziki wa Tanzania upo local sana, sasa hivi nimefanya mapumziko ya kufanya muziki kwa miaka miwili, kati ya hii miaka miwili niliyopumzika nimeona wasanii wengi kazi zao zimefanya vizuri lakini nikikuonyesha meseji utaona wanavyonipiga vizinga" amesema Rama Dee.