NEWS

10 Septemba 2020

Amber Lulu Amchana Uchebe, Asema ‘Muulizeni Shilole’


MSANII wa Bongo Fleva, Amber Lulu, amevunja ukimya na kuhusu stori zinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba ana mahusiano ya kimapenzi na aliyekuwa mume wa msanii mwenzake Shilole aitwaye Uchebe ambaye wameshaachana baada ya kutokea ugomvi baina ya wanandoa hao.



Trending stori hiyo inazungumziwa zaidi kwenye mtandao wa Instagram, ambapo juzi Amber Lulu aliamua kuweka ujumbe kwenye Insta Story yake akisema; “Acheni ujinga mimi na Uchebe wapi na wapi mxiuuu” lakini stori hazikuishia hapo, akawa kama ameuchochea moto kukoleza tetesi hizo.



Baada ya stori kusambaa sana na kuwa kubwa zaidi, Amber Lulu ameamua kusema haya: “Hayo ni mambo ya Instagram nimeshayazoea, hanipi shida pia sipendagi kuyaongelea, sijui hata yameanzia wapi na sina hata cha kuwaambia, hata nikisema niweke sawa suala hili wao itawasaidia nini kwanza hayo mambo ya Uchebe kamuulizeni Shilole.”