NEWS

11 Septemba 2020

Aunt Ezekiel: Shamsa Hajitambui



Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amesema kuwa msanii mwenzake Shamsa Ford hajitambui ndio maana anaongea mambo ya familia za watu bila kupewa ruhusa, hivyo yeye binafsi ameamua kumuacha na ujinga wake.



Akizungumza na Amani mwanamama huyo ambaye kwa sasa anatarajiwa kuitwa mama kwa mara nyingine tena, alisema kwamba siku zote katika maisha yake hawezi kubishana na mtu ambaye sio mstaarabu kwa sababu na yeye atakuwa hivyo.



“Siwezi kujibizana sana na Shamsa kwa sababu hajitambui, huwezi ukazungumza mambo ya watu tena ya ndani bila ruhusa ya wenyewe, halafu mambo yote aliyozungumza hana uhakika nayo, namuacha aendelee kuwa msemaji wangu sina muda wa kuhangaika naye,” alisema.



Siku za hivi karibuni Shamsa amekuwa akimrushia maneno Aunt mitandaoni akimsema kuhusu suala la kubeba ujauzito ambao mpaka sasa haijulikani baba mtoto wake.