NEWS

11 Septemba 2020

Q Chief awataja waliombadili kwenye muziki


Msanii wa BongoFleva Q Chief ameeleza kuhusu safari ya maisha yake kwenye muziki wakati alipokutana na msanii Jose Chameleone nchini Uganda ambapo alimpokea na kumuonyesha baadhi ya vitu walivyokuwa pamoja.



Akifunguka kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Q Chief amesema "Nilipokuwa nchini Uganda msanii chemeleone Jose alinikaribisha vizuri na kunizungusha kila kona, hii ilitokana na heshima na upendo tuliokuwa nao"

Aidha akizungumzia kuhusu maendeleo yake ya kimuziki tangu alipoanza hadi sasa amesema "Ustamiilivu ndiyo unanijenga kuwa imara siku zote, nimekutana na watu sahihi kama Daxo Chali na Marco Chali ambao wamefanya mabadiliko kwenye muziki wangu, nafanyia kazi Album yangu mpya na Tour yangu ambayo itakuja, kwa hiyo watu wajiandae kunipokea, mimi ni msanii ambaye napenda kuingia kwenye damu ya mtu na hiyo ndiyo maana ya mwanamuziki na muziki mzuri".

Q Chief ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao mpaka sasa wana heshima zao kwenye muziki na bado wanafanya muziki.