NEWS

12 Septemba 2020

China Kuondoa Tik Tok Marekani...


China imechukizwa na kauli ya Trump kuwa hafikirii kabisa kuongeza muda wa TikTok kuendelea kufanya shughuli zake Marekani ambapo Nchi hiyo imesema ni bora iondoe kabisa TikTok Marekani kuliko kukubaliana na ushauri wa Trump wa kuuza uendeshaji wa Mtandao huo wa Kichina kwa Wamarekani.


"Trump amesema mwisho Sept 15, 2020 ni bora muda ukifika tuondoke ila sio kuwauzia Wamarekani ambao wao wanataka kila kitu wakimilki wao bila kujua kuwa zama zimebadilika, kuwauzia itakuwa ni aibua kwa Mmliki wa TikTok ByteDance na China kwa ujumla" - CHINA