NEWS

13 Septemba 2020

Lebanon imeizuia ndege ya Uturuki kutua Beirut



Mamlaka nchini Lebanon imeizuia ndege ya mizigo ya Uturuki ambayo ilipaswa kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Rafik Hariri, baada ya ndege hiyo kupita katika eneo la anga la Israel.

Akinukuu vifungu vya sheria za Lebanon, Mkurugenzi wa uwanja wa ndege Fadi Al-Hassan amesema mamlaka ya uwanja wa ndege imeizua ndege hiyo kutua kwa vile ilifanya kosa la kupitia anga ya Israel, eneo la waloezi nchini Israel.

Hata hivyo aliongeza kusema hakuna matatizo zaidi na upande wa Uturuki na serikali ya Lebaon, imeelewa kwamba kitendo hicho kimetokea kwa makosa. Lebanon na Israel kwa hivi sasa zipo katika makabiliano ya kivita, na katika eneo la mpakani kumekuwa na hali ya kuongezeka kwa mvutano kati ya kundi la Hezbollah na jeshi la Israel.

Hezbollah lina uhusiano na hasimu mkubwa wa Israel, Iran. Na mwaka 2006 kulitokea vita vilivyodumu kwa mwezi mmoja kati ya kundi hilo la Isreal.