Mgombea Urais kupitia CHADEMA,Tundu Lissu katika kampeni zake zilizofanyika mkoani Morogoro leo Septemba 11,2020, amevitaja vipaumbele vyake ambavyo ni haki , usawa na maendeleo ya watu.
Akizungumza katika kampeni hizo amewataka wananchi hao kufanya maamuzi sahihi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu ili kupata Rais mwenye kujali uhuru na kuleta maendeleo.
“Niwaombe wana Morogoro muwachague viongozi waliobaki na ambao watarudishwa kwenye rufaa muwapigie kura ili mpate maendeleo” Lissu
“Sijapigwa risasi tu, nimepigwa kiuchumi, nilikua Mbunge na mnajua ulipoishia sasa hii kampeni tunaimalizaje inabidi tusaidiane, mimi nawaombeni mtuchangie sioni aibu” Lissu