NEWS

10 Septemba 2020

Museveni: Sihitaji kulumbana na vijana mitandaoni ili kuwashawishi, wengine wananiambia mimi mjinga



Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amekuwa akizungumzia mkakati anaotumia kuwavutia vijana katika mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na wale ambao “wananitukana ,wakisema, wewe ni mjinga sana”.

Alisema mkakati wake ni kufanya mijadala thabiti ili kuwashawishi wakosoaji wake.

“Sihitaji kulumbana na hawa watoto ili kuwashawishi, nikituma ujumbe kuwajibu kumi waliokuwa wakinishambulia, sita pekee wanabakia na wane wananijibu wakisema mzee ametoa hojanzuri.”

Bwana Museveni ameongoza Uganda tangu 1986 na atagombea urais kwa muhula wa sita katika uchaguzi mkuu ujao.

Miongoni mwa wale wanapanga kumpinga katika kinyang’anyiro hicho ni msanii aliyegeuka mwanasiasa Bobi Wine, 38, wambaye ni maarufu kwa vijana.