Watoto 10 wamepoteza maisha baada ya Shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyoko Kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani Kagera, kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2020.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa umri wa wanafunzi waliofariki ni kati ya miaka sita hadi 12.
Bweni lililoungua ni la wanafunzi wa kiume ambapo majeruhi 6 wamepelekwa Hospital ya Nyakahanga