NEWS

11 Januari 2014

Azimia baada ya Kuhojiwa na Jopo la Majaji Kwa tuhuma za Rushwa - Ni Bosi wa Uhamiaji

Mkurugenzi wa Uhamiaji nchini Kenya, Jane Waikenda jana alianguka kwenye ofisi za tume ya maadili na uzuiaji rushwa alikoenda kuhojiwa kutokana na utolewaji holela kwa vibali vya kuishi nchini humo.



Bosi huyo alipelekwa kwenye hospitali ya Nairobi. Picha hilo lilianza kwenye ofisi ya Waikenda iliyopo Nyayo House mapema asubuhi ya jana pindi wapelelezi wa EACC walipowasili kumhoji. Inadaiwa kuwa mama huyo alijifungua chooni.

Walinzi wake walizungumza na wapelelezi hao kuifanya kazi hiyo kwa njia nzuri..

Hatua ya kumhoji imekuja kufuatia kutolewa vibali 300 vya kufanyia kazi nchini humo ambavyo EACC inahisi kuna ‘magumashi’ yamefanyika. Vibali hivyo vilikuwa vya raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini humo.

Katika jengo la Integrity Centre, Waikenda anadaiwa kuzimia na alikimbizwa kwenye hospitali ya Nairobi alikolazwa.