NEWS

11 Januari 2014

Simba Yafuzu Fainali Mapinduzi Cup

Klabu ya Simba imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga URA ya Uganda mabao 2-0.


Mabao ya Simba kwenye mchezo huo yamefungwa na beki Joseph Owino pamoja na kiungo Amri Kiemba huku kiungo Owen Kasule wa URA akilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi Ramadhani Singano.
Simba sasa itacheza fainali siku ya Jumatatu na timu ya KCC pia toka nchini UGANDA iliyoitoa AZAM kwa mabao 3-2.

Chanzo: Shaffih Dauda