Kutokana na kiwango cha mchezaji huyo wa kati wa timu ya Man City na Ivory Coast, ambacho kimekuwa juu kwa muda mrefu ni sababu iliyomfanya mcezaji huyo kutwaa tuzo hiyo na pia mchango wake wakuweza kuifanikisha timu yake ya Taifa kufuzu kucheza mashindano ya World Cup yatakayofanyika South America Brazil.
Wachezaji wengine waliofanikiwa kutwaa tuzo hiyo mara tatu mfululizo ni Abedi Pele wa Ghana na Samuel Etoo wa Cameroon ambapo Etoo alichukua 2003-05 na kuchukua kwa mara ya nne 2010.